Hatma ya Maelfu ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Moi imesalia kwenye njia panda huku wahadhiri wa chuo hicho wakiapa kutorejea darasani licha ya kusitishwa kwa mgomo wa kitaifa wa wahadhiri wa vyuo vikuu vya umma. Wafanyikazi wa chuo hicho wakidai malimbikizi ya mishahara na wakitaka uchunguzi wa ubadhirifu wa fedha kufanywa.