Tume ya kupambana na ufisadi nchini imeanza uchunguzi wa ubadhirifu wa zaidi ya shilingi bilioni mbili katika chuo kikuu cha Jaramogi Oginga Odinga kaunti ya Siaya. Kulingana na malalamishi yaliyowasilishwa kwa tume hiyo ya EACC, sakata hiyo pia inahusisha sakata ya wanafunzi zaidi ya mia mbili kuhudhuria sherehe ya shahada ya uzamili licha ya kukosa kuhitimu.