Neema Gospel Choir, AICT Chang'ombe - NAPOKEA KIBALI (Official Video) 4K

Просмотров: 200, 577   |   Загружено: 6 год.
icon
Neema Gospel Choir
icon
812
icon
Скачать
iconПодробнее о видео
Mungu wetu ni mwaminifu, anaposema neno huwa habadiliki..
Muhimu ni kupokea kibali kutoka kwake tu.



Written by Fredrick Kilago
Performed by Esther Fredrick Kilago, Samuel Limbu & Josephine Peter
Produced by Neema Gospel Choir

Song Lyrics:
Nanyoosha mikono
Ninapokea kibali toka kwako
Sitaki kusita
Nazipokea nguvu za Roho wako


Mungu wa Israel
Hakuna Mungu ashikaye maagano
Kama wewe, kama wewe
Ninapenda kufanya maskani Karibu na wewe,
Kila saa, kila saa

Mungu ujuaye haja za moyo wangu Ee Yesu,
Uniponyaye mimi na nchi ya baba zangu
Huruma yako ni ya ajabu
Pendo lako linanivuta kwako Baba


Umeahidi kunisamehe
Na kuiponya nchi yetu Bwana
Iwapo watu wako
Tulioitwa kwa jina lako
Tutajinyenyekesha mbele zako

Na kuziacha njia zetu mbaya
Na kuutafuta uso wako Utasikia toka mbinguni
Na kuiponya nchi yetu Bwana


Ewe Yesu wangu, Ewe Bwana
Napondeka najitoa kwako Niwe wako, niwe wako
Niwe wako milele


Kabla ya kutazama mbele yetu
Hebu tuangalie ni wapi Mungu ametutoa?
Ni mangapi Mungu ametuvusha?
Na kama si Mungu tungekuwa wapi leo?

Wapo wengi waliotamani kuwa hivi tulivyo
Lakini hawakupata hiyo neema
Lakini sisi Mungu ametupa kibali
Na ameahidi kuwa nasi mpaka ukamilifu wa Dahari
Ahadi zake ni kweli na amini

Wakati huu tukiwa katika uwepo wa Mungu,
unayo nafasi mwenyewe ya kumwambia
Mungu akupe kibali Kibali katika kazi yako,
kibali katika familia yako, kibali katika biashara yako

Mwambie Mungu maneno ya kinywa changu na
mawazo ya moyo wangu yapate kibali mbele zako,
Mwambie Bwana autawale moyo wako,
jimimine mbele za Bwana,

Mwambie Bwana kama ayala ayatamanivyo maji ndivyo nafsi yangu na zaidi Jehova yakutamani wewe,
ninahitaji nikae na wewe, ninahitaji nitembee na wewe, nikae nyumbani mwako, nitafakari uzuri wako, hekaruni mwako

Bwana nakutamani niongoze maisha yangu Bwana, peke yangu siwezi. Mwambie Bwana akufanye uwe wake Haleluya


Ewe Yesu wangu, Ewe Bwana Napondeka najitoa kwako Niwe wako, niwe wako

Niwe wako milele


Contacts:
Email: neemagospelchoir@gmail.com
Phone: +255 756 777 288
Whatsapp: +255 756 777 288
Telegram: t.me/neemagospeltz
Facebook: Neema Gospel Choir
Instagram: neema_gospel_choir
Twitter: Neema Gospel Choir

Похожие видео

Добавлено: 56 год.
Добавил:
  © 2019-2021
  Neema Gospel Choir, AICT Chang'ombe - NAPOKEA KIBALI (Official Video) 4K - RusLar.Me