
Pata ujumbe wenye kugusa moyo kwamba licha ya changamoto, kimbilio letu na msaada wetu vinabaki kwa Yesu pekee.
Wimbo huu uvuvie imani yako na ufanye upya tumaini lako kwa Mungu.
Songwriter & Composer: Godwin Mlambo
Leader: Loyce Simon
Video Editor: Enock Magwesela
LYRICS
Nianze na wewe,
nimalize na wewe
Safari yangu niongozwe nawe
Ukiniacha nitapotea Bwana
Ukiniacha nitaangamia
Ukiniacha nitapotea Bwana
Usiruhusu yatokee haya
Kimbilio langu umebaki mwenyewe
Msaada wangu umebaki mwenyewe
Wewe tu, wewe tu
Bado ninakuamini